NJIA YA MAANDISHI

MAANDISHI
       Njia hii imeimeza fasihi simulizi kwa manufaa ya baadae. Ugunduzi wa alama za uandishi ndio uliopelekea fasihi simulizi kuhifadhiwa katika maandishi. Leo hii ni vigumu kuifahamu kazi ya fasihi simulizi iliyowekwa kwenye maandishi. Njia pekee ya kuipambanua ni kuangalia tabia za fasihi simulizi ambazo ni: “paukwa…pakawa”au “hadithi….hadithi njoo
       UBORA WA UHIFADHI WA MAANDISHI
•Ni njia nzuri kwa kutunza kumbu kumbu kwa vizazi vijazo
•Kazi iliyo huifadhiwa katika maandishi inaweza kufikahata hadhira iliyopo mbali
•Kazi iliyo hifadhiwa katika maandishi haiwezi kubadilika fani na maudhui yalio kusudiwa

UDHAIFU/ATHARI YA UHIFADHI WA MAANDISHI
• Uhifadhi kwa maandishi huwa na matatizo yafuatayo:
• Kukosekana kwa utendaji,sauti,kuimba vitabia.
• Kukosekana kwa uhusiano wa moja kwa moja kati ya hadhira na fanani
• Kukosekana kwa mabadiliko ya mara kwa mara.
• Ufinyu wa hadhira, itakuwa na watu wachache tu, wale wanaojua kusoma na kuandika.
• Inakuwa ni nyenzo ya kibiashara ambapo inahitaji kugharamiwa.

No comments:

Post a Comment