SIFA ZA FASIHI SIMULIZI

SIFA ZA FASIHI SIMULI

Fasihi simulizi ina sifa za pekee zinazoweza kutofautisha na aina nyingine ya fasihi. Sifa
hizo ndizo huipa uhai fasihi hii. Miongoni mwa sifa hizo ni pamoja na:

 •Utendaji; Fasihi simulizi huwa na utendaji, yaani vitendo halisi hupatikana. Utendaji
wa fasihi simulizi hushirikisha fanani na hadhira kwa wakati mmoja.
 • Uwepo wa fanani na hadhira; Fasihi simulizi hukutanisha fanani na hadhira kwa
wakati mmoja- Fanani huweza kusimulia, kupiga makofi na hata kubadilisha miondoko
na mitindo ya usimuliaji. Hadhira huweza kushiriki kwa kuuliza maswali, kupiga
makofi, kushangilia kuimba na kadhalika kutegemeana na jinsi ambavyo fanani
atawashirikisha.
•Huwasilishwa kwa njia ya mzungumzo ya mdomo.
•Huifadhiwa kichwani; asili ya fasihi simulizi ni kuhifadhiwa kichwani na kirithishwa kutoka kizazi kimoja hadi chengine kwa njia ya masimulizi.
• Humpa uhuru msanii wa kufanya mabadiliko kwa kuzingatia mazingira na uhitaji; masimulizi anaweza kubadilisha masimulizi kulingana na rika,wakati,na mazingira aliyopo bila ugumu wowote.
•Huwa ni mali ya jamii nzima; Kila mmoja anahaki ya kumiliki kazi ya fasihi simulizi bila kikwaz cha aina yoyote na kuitumia katika mazingira yake.
•Huwa na wakati maalum na pahala maalum pa kuiwasilisha.
• Huruhusu viungo vingine vya mwili kutumika katika uwasilishaji.
•Huwa inaruhusu hadhira kushiriki katika uwasilishaji wake.
Uwepo wa fanani na hadhira

No comments:

Post a Comment